• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Bwawa la Nyerere kuisha haitakuwa sababu ya kupungua kwa bei ya Umeme

Bynijuzetz

Jul 27, 2023

Licha ya gharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka kama ambavyo hayati John Pombe Magufuli alivyowaahidi watanazania kipindi cha uhau wake, baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, Tanesco wamebainisha kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.

Bwawa hilo linatarajia kuzalisha megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.

Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na Msajili wa Hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.

Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.

“Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda,” amesema.

Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.

Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.

Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.

Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.

Kuhusu bwawa la Nyerere

Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.

Leave a Reply