• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Wimbo wa Nay wa Mitego wamfikisha BASATA kujadidili maudhui

Bynijuzetz

Jul 27, 2023

Kazi ya sana a ni kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya mambo ya kijamii, kufurahisha na hata kukosoa pale jamii inapokuwa imepotoka hususani kwenye mambo ya msingi na kimaadili, mfano Rushwa, uongozi mbovu, Uzembe na hata kutokujituma kwa baadhi ya vijana.

Je, hili lina uzito gani kwa jamii zetu nchini Tanzania? Tafsiri yake ni ipi hasa pale ukosoaji unapogusa sehemu za juu za uongozi wa serikali?

Je, ni kweli sanaa yetu haiko huru kuusemea Umma hasa pale viongozi wetu wanapokosea wasionywe wala kukanywa ili kulinda heshima zao ilihali wananchi wa tabaka la chini wakiwa kwenye maumivu makali? Kama ni kweli kazi ya sanaa ni ipi au ni kuburudisha kwa hofu kwa kuhofia asasi za kiserikali kuifunga mdomo sanaa?

Ni msanii kutokea Bongo Fleva Emmanuel Elibariki, Nay wa Mitego ambae leo ameutaarifu umma kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa ameitwa na Baraza la Sanaa Tanzania.

Sasa yakaibuka maswali yasiyo na majibu Je ni kutokea na wimbo wake aliouachia hivi karibu ama ni nini, sasa Millardayo.com & Ayo TV imempata kwa njia ya simu…

Wameniambia nahitajika Kwenye kikao Asubuhi Ya leo saa nne, kujadili wimbo wangu wa Amkeni, Barua imenifikia leo Asubuhi na walikuwa wanataka niende Asubuhi Ya leo leo Sasa huoni kama kitu kidogo hakiko sawa na Kwa bahati mbaya mimi nimesafiri, Mwanasheria amewasiliana nao Nadhani kama kutakua na ratiba mpya ya kikao nitahudhuria,  nahisi kurudi Jumatatu, wimbo wangu hauna ukakasi, ukiona mpaka wimbo nautoa umeshapitiwa na watu wengi ushaeditiwa sana mpaka unatoka”

Sema tu Kwa Sababu watu hawapendi ukweli, ni wimbo ambao nimezungumza Maisha ya kila mtu, Ukumbuki utaratibu wa kupeleka wimbo usikilizwe kwanza ushatolewa, ilikuwa sio lazima, tutaangalia siku hiyo itakavyokua, mimi nafanya kwaajili ya Jamii yangu” Nay wa Mitego

Leave a Reply