• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Gerald Hando: Watanzania wengi ni maamuma kuhusu mkataba wa Bandari

Bynijuzetz

Jul 28, 2023

Mtangazaji wa Kipindi cha Good morning kinachorushwa kwenye kituo cha Wasafi FM Gerald Hando amesema asilimia 99 ya wanaojadili sakata la mkataba wa uwekezaji Bandarini unaohusisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mamlaka ya usimamizi wa Bandari na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya DP World ni Maamuma (Mambumbumbu) akiwemo yeye mwenyewe kwakuwa wamekuwa watu wa kulishwa maneno na kuyarudia bila kujuwa undani wa wanachokijadili.

Hando ameyasema hayo leo Asubuhi, Ijumaa Julai 28.2023 wakati timu ya kipindi hicho ikiwa kwenye mahojiano maalumu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala, mahojiano yaliyofanyika Jijini Mwanza yakilenga kusindikiza ubunifu unaofanywa na kituo hicho kuwafuata Wakuu wa mikoa kwenye maeneo yao ili kutambua fursa za uwekezaji zilizopo kwenye eneo husika, fursa zilizopewa jina la Wekeza na Samia.

Kwa upande wake Makala akizungumzia suala hilo linalozidi kutengeneza mjadala kila uchwao amesema kuwa mipango ya uboreshaji Bandarini haijaanza sasa na kwamba anaamini kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kujitokeza kupinga maboresho yanayopaswa kufanywa Bandarini ila kinachotokea sasa ni utengenezaji wa propaganda ambayo imeambatana na uongo mkubwa wenye chembe kidogo za ukweli na kisha uwongo huo unarudiwarudiwa na wapingaji, na kwamba kinachopelekea Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka hadharani kukanusha ni kwasababu uwongo ukiachwa ushamiri unakuwa kweli kwakuwa kwenye suala la propaganda anayesema mwisho ndiye anayehesabiwa kuwa mkweli

“…Kwahiyo ukiacha Makala mwizi ukaa kimya watu wanaamini wewe mwizi, Kwahiyo kwenye hili watu wanatumia zile chembechembe ndo maana wanakuuliza ukomo wa muda eeeh.., sasa anasoma hiki halafu hamalizii, eeeh.. imeuzwa, mule ukiangalia hakuna sale agreement… kwamba watu wameuza Bandari, lakini mtu anakuambia na Bandari zote zimeuzwa…”

Amesema mkakati mkubwa wa propaganda ni lazima uzue hofu, taharuki na udanganyifu na ndicho kinachofanywa na wale wanaopinga mpango huo wa serikali lakini uhalisia uliopo ni kwamba Bandari inatakiwa kufanyiwa maboresho kutokana na miundombinu iliyopo.

Leave a Reply