• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Urusi kusimamia Usafirishaji wa nafaka kwa bara la Afrika bila malipo

Bynijuzetz

Jul 28, 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameeleza nia yake ya kutuma nafaka katika mataifa sita ya Afrika bila malipo.

Putin alisema hayo katika mkutano kati ya Urusi na nchi za Afrika mjini St Petersburg.

Katika mkutano huo rais Putin alisema katika miezi michache ijayo wataanza kutuma nafaka bure.

Haya yanajiri baada ya Urusi kujiondoa katika makubaliano ya Bahari Nyeusi na Ukraine mapema mwezi huu.

Putin alisema kuwa Urusi iko tayari kujaza upungufu wowote wa nafaka unaosababishwa na Ukraine.

Alisema na kuongeza kuwa Urusi iko tayari kusambaza nafaka kwa nchi sita za Afrika katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo.

Alisema, “Katika muda wa miezi mitatu hadi minne ijayo, Urusi itatuma tani 25,000 hadi 50,000 za nafaka kwa kila nchi.

Nchi hizo ni Burkina Faso, Zimbabwe, Mali, Somalia, Afrika ya Kati, na Eritrea.

Putin alisema, “Tutahakikisha pia kwamba hazinatumwa bure bila kulipa ada yoyote ya usafirishaji.”

Leave a Reply