• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Nijuze inakujuza leo juu ya kazi ya Uhudumu wa ndege, fuatilia makala hii

Bynijuzetz

Jul 31, 2023

Kazi ya uhudumu wa ndege mara nyingi inaonekana kuwa ya kupendeza na ya kusisimua, yenye fursa za kusafiri ulimwenguni na kukutana na watu kutoka tamaduni tofauti lakini pia ina mapungufu yake.

Hapa kuna baadhi ya vipengele vyeusi zaidi vya kazi husika.

Saa nyingi za kazi

Wahudumu wa ndege mara nyingi hulazimika kufanya kazi kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na usiku, wikendi na likizo.

Ratiba ya kazi inaweza kuwa isiyo ya kawaida na kukosa usingizi na uchovu uliopitiliza.

Malipo hafifu

Ingawa baadhi ya mashirika ya ndege hulipa wafanyakazi wao vizuri, mengi hayawalipi vizuri, hasa kwa wale wanaoanza kazi, malipo yanaweza kuwa ya chini kabisa.

Mifadhaiko na Shinikizo

Kazi hii inaweza kuwa yenye mfadhaiko (stress) na shinikizo (pressure) hasa kukiwa na hitaji la kushughulikia abiria wasio na uelewa (vichwa ngumu), kushughulikia ucheleweshaji wa ndege au mabadiliko na kuhakikisha usalama wa abiria katika hali za dharura.

Upweke na Mtengano

Kuwa mbali na nyumbani kwa muda mrefu kunaweza kusababisha hisia za upweke na kutengwa.

Hii inaweza kuwa changamoto hasa kwa wale walio na familia na mara nyingine kukosa matukio muhimu kama sherehe, vikao, sikukuu n.k

Kikomo cha kazi

Ingawa kuna fursa za kujiendeleza, mara nyingine hizi kazi huwa na vikwazo, na upandishaji vyeo unaweza kuchukua muda mrefu.

Mtindo usio bora Kiafya

Kufanya kazi saa zisizo za kawaida, kusafiri mara kwa mara, ulaji wa vyakula vya aina moja kunaweza kusababisha athari ziszofaa kiafya.

Unyanyasaji wa kijinsia na Ubaguzi

Kwa bahati mbaya, hili ni tatizo katika tasnia nyingi, na tasnia ya usafiri wa anga pia hutokea suala la ubaguzi wa kimuonekano na unyanyasaji wa kijinsia hasa wanawake, wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji kutoka kwa abiria au wafanyakazi wenza.

Viwango madhubuti vya muonekano

Mashirika mengi ya ndege yanazingatia madhubuti kuhusu mwonekano wa wafanyakazi wa Ndege zao, jambo ambalo linaweza kusababisha kukosekana kwa usawa wa kazi kwa kuangalia sura na mwili.

Tambua kwamba sababu hizi zinaweza kutofautiana kutegemea na shirika na nchi hadi nchi.

Leave a Reply