• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Tanzia: DJ Steve B aliyewahi kufanya kazi Clouds Media afariki dunia

Bynijuzetz

Jul 31, 2023

Aliyewahi kuwa DJ wa CloudsFM Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia leo katika Hospitalini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa presha.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu amezungumza na moja ya media kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali juzi na kuwekwa ICU baada ya presha kupanda na baadaye kupanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

“Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya leo saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini figo sio chanzo cha kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383”

“Steve hakuwa na Mke wala hajaacha Mke na wala Mtoto, hatuna taarifa za Mtoto wake” ——— amemalizia Armstrong Mdoe.

Leave a Reply