• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Brand ya nguo ya “SleekSingh” yazidi kuwatamanisha wapenzi wa fashion

Bynijuzetz

Aug 1, 2023

Ikiwa ni siku chache toka brand mpya ya nguo kutangaza kuja na Ubunifu wa nguo za ndani na vifaa vya michezo, sasa moja moja kat ya wabunifu wa mavazi kutoka brand hiyo ametujuza kuwa wao wameandaa vitu vyenye kiwango cha juu huku wakianza na saizi ndogo “S”, saizi ya kati “XL” pamoja na ile kubwa ya wastani “L”.

Ameidokezea nijuze kuhusu utaratibu wa mauzo pamoja na Stoo ambazo watakuwa kama wasambazaji wakuu wa brand hiyo.

“Kwa upande wa mauzo,sisi tuna wasambazaji kadhaa ndani ya Dar es Salaam ambao tayari tumeshaweka nao biashara mezani ambao wao biashara zao zinahusu pia maduka yao ya mikoani pia kama kuna wengine sisi tuko wazi kupokea maombi na kukaa mezani kwa mazungumzo ya kibiashara ili kusukuma gurudumu la biashara kwa pamoja”

Tunapenda kuwataarifu watanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wakae tayari kwaajili ya kupokea bidhaa zetu ikiwemo mapokezi ya Jezi mpya za klabu ya Coastal Union ” Wagosi wa Kaya”

Leave a Reply