• Mon. Feb 26th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mkuu wa mkoa wa Mara atembelea na kutoa pole eneo la tukio, Sehemu inayodaiwa mtumbwi kuzama

Bynijuzetz

Aug 1, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda amefika katika Kijiji cha Mchigondo wilayani Bunda Mkoani Mara kutoa pole kwa wananchi kutokana na tukio la watu 13 kuzama Maji katika ziwa Victoria.

“Naomba mpokee pole pia kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko pamoja na sisi katika tukio hili la kusikitisha ambalo limetupata wana Mara kwahiyo tuendelee kuwa watulivu tunaimani tutawapata wapendwa wetu”Said Mtanda Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt.Vicent Naano amesema kuwa hadi sasa mtu mmoja kati ya 13 wanaotafutwa amepatikana.

“Hadi sasa Kati ya watu 13 ambao tulikuwa tunawatafuta tumeshapata watu wa wili (2) hivyo bado tunatafuta watu 11 sasa tunawashukuru sana Wananchi wamekuwa watulivu na wanatoa ushirikiano katika shughuli nzima”Dkt Vincent Naano Mkuu wa Wilaya ya Bunda.

Leave a Reply