• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Niger: Mfanyabiasha atoa sababu za kuitaka Urusi na si Ufaransa

Bynijuzetz

Aug 1, 2023

Katika ishara ya kuongezeka kwa uhasama dhidi ya nchi za Magharibi tangu mapinduzi ya Niger, mfanyabiashara anaonesha mavazi yake yenye rangi ya bendera ya Urusi katika eneo la jadi la Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Tangu mapinduzi hayo, kumekuwa na vita vya maneno kati ya jeshi na nchi za Magharibi.

Bw Bazoum alikuwa mshirika mkubwa wa nchi za Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kijihadi, na pia alikuwa mshirika mkubwa wa kiuchumi.

Niger ina kambi ya kijeshi ya Ufaransa na ni nchi ya saba kwa uzalishaji wa urani duniani. Mafuta hayo ni muhimu kwa nishati ya nyuklia huku robo yake ikienda Ulaya, hasa ukoloni wa zamani wa Ufaransa.

Tangu Jenerali Abdourahamane Tchiani alipomuondoa madarakani rais katika mapinduzi ya Julai 26, rangi za gebdera ya Urusi zimeonekana ghafla mitaani.

Maelfu ya watu walishiriki maandamano katika mji mkuu Niamey siku ya Jumapili, huku baadhi wakipeperusha bendera za Urusi na hata kushambulia ubalozi wa Ufaransa.

Sasa inaonekana “harakati” hii inaenea kote nchini.

Mfanyabiashara huyo, anayeishi umbali wa kilomita 800 (maili 500) katikati mwa jiji la Zinder, hakutaka kutaja jina lake kwa sababu za usalama na kuomba tufiche uso wake.

“Mimi ni mtetezi wa Urusi na siipendi Ufaransa,” alisema. “Tangu utotoni, nimekuwa nikipinga Ufaransa.

“Wamenyonya utajiri wote wa nchi yangu kama vile uranium, petroli na dhahabu. Watu masikini zaidi wa Niger hawawezi kula chakula mara tatu kwa siku kwa sababu ya Ufaransa.”

Mfanyabiashara huyo alisema maelfu wameshiriki maandamano ya Jumatatu huko Zinder kuunga mkono unyakuzi wa kijeshi.

Alisema alimwomba fundi cherehani wa eneo hilo kuchukua nyenzo za rangi za Kirusi za nyeupe, bluu na nyekundu na kumtengenezea vazi hilo, akikana kwamba lilikuwa limelipwa na vikundi vinavyounga mkono Urusi.

Niger ni makazi ya watu milioni 24.4 ambapo wawili kati ya watano wanaishi katika umaskini uliokithiri, chini ya dola 2.15 kwa siku.

Waandamanaji

Rais Bazoum aliingia madarakani mwaka 2021 katika kipindi cha mpito cha kwanza cha kidemokrasia na amani cha uongozi wa Niger tangu uhuru mwaka 1960.

Lakini serikali yake ilikuwa inalengwa na wanamgambo wa Kijihadi wanaohusishwa na kundi la Islamic State na al-Qaeda ambao wanahudumu katika maeneo ya Jangwa la Sahara na Sahel upande wa kusini.

Chini ya shinikizo kutoka kwa Waislam, majeshi katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso, pia makoloni ya zamani ya Ufaransa yenye maslahi makubwa ya Ufaransa, yalichukua mamlaka katika miaka ya hivi karibuni, akisema hii itasaidia katika vita dhidi ya wanajihadi.

Kama vile Niger, nchi hizi zote mbili hapo awali zilikuwa na idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa wanaowasaidia lakini wakati mashambulizi ya wanamgambo yakiendelea, hisia za chuki dhidi ya Ufaransa ziliongezeka katika eneo hilo, huku watu katika nchi zote tatu wakianza kuwashutumu Wafaransa kwa kutofanya vya kutosha kuwazuia.

Mara baada ya kuchukua utawala, jeshi nchini Mali lilikaribisha kundi la mamluki la Wagner la Urusi walipowalazimisha kwanza wanajeshi wa Ufaransa na kisha kushinikiza maelfu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuondoka.

Ingawa mashambulizi ya Kiislamu yameendelea nchini Mali, serikali ya Burkina Faso pia imekua karibu na Urusi na kuwafukuza mamia ya wanajeshi wa Ufaransa.

Nchini Niger, maandamano dhidi ya Ufaransa yalipigwa marufuku mara kwa mara na utawala wa Bw Bazoum.

Mashirika kadhaa ya kiraia yalianza kushadidi maandamano dhidi ya Wafaransa katikati ya mwaka wa 2022, wakati utawala wa Bw Bazoum ulipoidhinisha kutumwa tena kwa wanajeshi wa Ufaransa wa Barkhane hadi Niger baada ya kuamriwa kuondoka nchini Mali.

Muhimu miongoni mwao ni vuguvugu la M62, lililoundwa mwezi Agosti 2022 na muungano wa wanaharakati, vyama vya kiraia na vyama vya wafanyakazi. Waliongoza wito dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha, utawala mbovu na uwepo wa vikosi vya Ufaransa.

Rangi za bendera ya Urusi zimeonekana ghafla kwenye mitaa ya Niger
Maelezo ya picha,Rangi za bendera ya Urusi zimeonekana ghafla kwenye mitaa ya Niger

Maandamano mbalimbali yaliyopangwa na kundi hilo yalipigwa marufuku au kukabiliwa vikali na mamlaka ya Niger huku kiongozi wake Abdoulaye Seydou akifungwa jela miezi tisa Aprili 2023 kwa “kuvuruga utulivu wa umma”.

M62 inaonekana kuimarika kufuatia kuondolewa kwa Rais Bazoum.

Katika hali isiyo ya kawaida, wanachama wake walinukuliwa na runinga ya taifa wakihamasisha maandamano makubwa ya kuunga mkono utawala wa kijeshi, pamoja na kulaani vikwazo vilivyowekwa na viongozi wa Afrika Magharibi kutokana na mapinduzi hayo.

Haijulikani ikiwa kikundi hicho kinahusishwa na serikali ya kijeshi inayojulikana kama Baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi (CNSP) au na Urusi.

Lakini lilikuwa ni kundi mwamvuli lililoandaa maandamano ya Jumapili, ambapo makundi madogo ya kiraia kama vile Kamati ya Uratibu ya Mapambano ya Kidemokrasia (CCLD) Bukata na Youth Action for Niger pia walikuwepo.

Huko Zinder, mfanyabiashara anayeiunga mkono Urusi ana maoni chanya kuhusu jinsi Moscow inaweza kusaidia nchi yake.

“Nataka Urusi kusaidia kwa usalama na chakula,” alisema. “Urusi inaweza kusambaza teknolojia ili kuboresha kilimo chetu.”

Lakini Moutaka, mkulima ambaye pia anaishi Zinder, anakataa hoja hii na kusema mapinduzi hayo ni habari mbaya kwa kila mtu.

“Siungi mkono ujio wa Warusi katika nchi hii kwa sababu wote ni Wazungu na hakuna mtu atakayetusaidia,” alisema. “Ninaipenda nchi yangu na natumai tunaweza kuishi kwa amani.”

Leave a Reply