• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Wiki ya asasi zisizo za kiserikali yazinduliwa Dar es Salaam

Bynijuzetz

Aug 2, 2023

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndungulile amezitaka asasi za kiraia kuwa vinara wa kutoa mtazamo mbadala kuhusu miswada inayowasilishwa ili kuwasaidia wabunge kufanya maamuzi sahihi.

 Ndugulile amesema kazi hiyo kufanywa katika hatua za awali kabla ya muswada kuwa kwenye hatua za mwisho za kupitishwa na Bunge ili kupunguza manung’uniko maamuzi yanapofanyika.

Mbunge huyu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa mada kwenye uzinduzi wa juma la asasi za kiraia linalotarajiwa kuanza Agosti 7 jijini Arusha.

“Wabunge tunazitegemea asasi za kiraia kutuwezedha kupata mtazamo mbadala pale miswada inapoletwa. Bahati mbaya mnakuja kwa kuchelewa hata maoni yenu yanakuwa hayafanyiwi kazi.

“Ningewaomba muwe na masikio na pua za kunusa, kila mnaposikia kuna muswada kabla haujaletwa bungeni fanyeni utafiti mtoe maoni yenu mapema,” amesema Ndugulile.

Mbunge huyo ambaye pia amewahi kuhudumu kwenye baraza la mawaziri ametumia fursa hiyo kuzitaka asasi za kiraia kutoka kwenye dhana ya uanaharakati na kuwa taasisi zinazotoa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Asasi za Kiraia (FCS) Francis Kiwanga amesema juma hilo la asasi za kiraia linafanyika kwa mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.

Amesema lengo la juma hilo ni kuziwezesha asasi hizo kukutana na kuweka mipango ya pamoja katika kuhakikisha zinatimiza wajibu wake kwa jamii na lengo la kuanzishwa kwake.

Kauli mbiu ya juma la asasi za kiraia mwaka huu ni ‘Teknolojia na jamii tulipotoka, tulipo na tunapoelekea’.

Leave a Reply