• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Dk Mwinyi aainisha juu ya Utambuzi wa Serikali kwa waandishi wa Habari Wanawake

Bynijuzetz

Aug 3, 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi wa fani mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, uboreshwaji wa miundombinu, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano.

Ameyasema hayo leo akifungua Kongamano la nane la Wahandisi Wanawake Tanzania (TAWECE)

Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wahandisi hasa Wanawake na mafundi sanifu.

Vilevile, Serikali itahakikisha inawasaidia Wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu ya Sekondari, Vyuo vya mafunzo ya amali na Vyuo Vikuu katika hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake nchini.

.
.

Leave a Reply