• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mwenge wa Uhuru wamaliza kukimbizwa kwa kuzindua miradi 41 Shinyanga

Bynijuzetz

Aug 4, 2023

Mwenge wa Uhuru uliomaliza kukimbizwa mkoani Shinyanga umekagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 41 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh41 bilioni katika wilaya tatu za mkoa huo.

Pamoja na miradi ya maendeleo, mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga pia ziliambatana na kuhamasisha wananchi kupima kwa hiari Virusi vya Ukimwi ambapo watu 1,495 walijitokeza kupima, miongoni mwao, wanaume wakiwa 992 na wanawake 503.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme wakati wa hafla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, jumla ya watu 13, sawa na asilimia 0.9 ya watu 1, 495 waliopimwa wamebainika kuambukizwa VVU.

Kuhusu miradi ya maendeleo, RC Mndeme amesema miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya Sh7 bilioni imewekewa mawe ya msingi huku miradi mingine yenye thamani ya zaidi ya Sh30 ikikaguliwa na kuzinduliwa.

‘’Nawashukuru viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa maagizo, ushauri na maelekezo; mimi binafsi kwa kushirikiana na viongozi wote mkoani Shinyanga tutahakikisha tunazingatia na kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na kiongozi wa Mwenge,’’ amesema Mndeme

Joseph Masalu, mkazi wa Msalala amepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwasihi viongozi wenye dhamana ya utekelezaji na usimamizi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ubora kulingana na tahamni halisi ya fedha za umma zinazotumika.

Leave a Reply