• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Shirika la madini la Taifa (Stamico) lanyakua tuzo Kimataifa

Bynijuzetz

Aug 8, 2023

Juhudi za Serikali kuinua sekta ya madini nchini zimeanza kuzaa matunda baada ya Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kunyakua tuzo ya Kampuni bora ya mwaka Afrika kwenye sekta ya madini 2023 katika tuzo za Africa Company of the Year Award (ACOYA).

 Tuzo hiyo iliyolewa mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuifanya Tanzania kuweka historia ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kubeba tuzo hiyo ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza nchini.

Mchakato wa kutafuta washindi umefanywa na Kampuni ijulikanayo kama Eastern Star Consulting Group Afrika iliyopo nchini Kenya.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya shirika, Mkurugezi Mtendaji, Dk Venance Mwasse ambaye aliambatana na menejimenti ya shirika hilo alisema tuzo hiyo imedhihirisha juhudi za shirika hilo katika kuinua sekta ya madini nchini.

Alisema hatua ya Stamico kuwa kampuni bora kwa mwaka 2023 imekuwa chachu kwa shirika hilo kuongeza kasi ya utendaji ili kuwanufaisha Watanzania.

“Zaidi ya nchi 15 kutoka bara la Afrika zilishiriki kwenye kuwania tuzo hizi na Stamico iliweza kuibuka kidedea kama kampuni bora ya madini Afrika,” alisema.

Stamico  imekuwa mfano wa kuigwa Afrika kiasi cha kuivutia wizara ya madini na Uchumi wa Bluu nchini Kenya ambayo hivi karibuni viongozi waandamizi wa wizara hiyo walikuja nchini kujifunza namna shirika hilo linavyoendeleza shughuli  za mnyororo  wa thamani wa uchimbaji madini.

Walijifunza namna Stamico imefanikiwa katika kuendesha shughuli za madini zikiwemo utafiti, uchimbaji, uchakataji, na biashara ya madini 

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Mkurugenzi wa Africa Company of The Year Awards (ACOYA), Deogratius Kilawe alisema tuzo hizo zinajulikana kama Africa Company of the year Awards (ACOYA), mwaka huu 2023 ndio mara ya kwanza tuzo hizo kutolewa hapa Tanzania.

Kilawe alizipongeza na kuzishukuru kampuni zote zilizoshiriki na kushinda.

Alisema lengo la tuzo hizo ni kuongeza ufanisi kwa kampuni katika utoaji huduma kwa wateja wao na wafanyakazi ili kuongeza uwajibikaji kazini.

“Mwisho wa tuzo hizi ni mwanzo wa maandalizi wa tuzo zijazo tunachukua changamoto zilizojitokeza mwaka huu kuboresha tuzo zijazo,

Mbali na Stamico kupata tuzo katika hafla hiyo kuna baadhi ya kampuni nyingine ziliweza kupata tuzo kama vile kampuni ya Ndege ya Uganda (Uganda Airlines) ambayo iliibuka kama Kampuni ya bora barani Afrika (Best Airline of the Year) na Kampuni ya Kenya Wee Centre ilibuka mshindi wa kwanza kwa utunzaji wa mazingira na Kampuni ya Sintel Security ya nchini Kenya iliibuka mshindi kwenye kipengele cha uchapishaji nyaraka mbalimbali (printing solutions).

Leave a Reply