• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Benki ya dunia imetangaza kusitisha ufadhili wa miradi ya Umma baada ya kupitisha sheria inayopinga Ushoga

Bynijuzetz

Aug 9, 2023

Benki ya Dunia imetangaza kusitisha kufadhili wa miradi ya umma nchini Uganda, baada ya taifa hilo kupitisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

 Kwa mujibu wa tovuti ya Taifa Leo, benki hiyo ilifikia uamuzi huo baaada ya kushinikizwa na makundi ya kutetea haki za wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja pamoja na Bunge la Congress la Marekani.

“Sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja ya Uganda kimsingi inakinzana na maadili ya kundi la Benki ya Dunia. Tunaamini maono yetu ya kutokomeza umaskini duniani yanaweza tu kufanikiwa ikiwa yanajumuisha kila mtu bila kujali rangi, jinsia,” Benki ya Dunia imesema kwenye taarifa yake iliyotolewa jana Agosti 8, 2023 na kuongeza;

“Sheria hii inadhoofisha juhudi hizo. Kujumuika na kutobaguliwa ndio msingi wa kazi yetu kote ulimwenguni.”

Benki hiyo imesema baada ya sheria hiyo kutungwa, ilituma timu nchini humo kukagua jalada lao katika muktadha wa sheria hiyo mpya na kubaini hatua za ziada kuchukuliwa ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vyao vya mazingira na kijamii.

“Lengo letu ni kulinda walio wachache dhidi ya ubaguzi na kutengwa katika miradi tunayofadhili. Hatua hizi kwa sasa zinajadiliwa na mamlaka.

“Hakuna ufadhili mpya wa umma kwa Uganda utakaowasilishwa kwenye Bodi yetu ya Wakurugenzi Watendaji hadi hatua za ziada ztakapochukuliwa,” imesisitiza benki hiyo.

Leave a Reply