• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

China na Tanzania zaendelea kushirikiana katika sekta ya Nishati ili kuinua uchumi

Bynijuzetz

Aug 14, 2023

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuwekeza katika kutekeleza miradi ya sekta ya nishati nchini. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa China, Liao Min wakati alipokutana na Waziri wa Nishati January Makamba, Agosti 14, jijini Dar es Salaam na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano katika uwekezaji na uendelezaji wa miradi ya sekta ya nishati inayofadhiliwa na China.

“China imewezesha utekelezaji wa miradi zaidi ya 11, ikiwemo ujenzi wa kuimarisha Gridi ya Taifa kwa Ukanda wa Kaskazini na Mashariki, ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania( EACOP), kituo cha kupoza na kupokea umeme cha Chalinze na maeneo mbalimbali nchini” January Makamba, Waziri wa Nishati akiongea na Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa China, Liao Min leo Agosti 14, 2023

Leave a Reply