• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Serikali kutumia helikopita ili kufukuza tembo katika makazi ya watu

Bynijuzetz

Aug 14, 2023

Kufuatia kifo cha mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Said Kuleni katika Kijiji cha Narungombe, Kata ya Mkoka wilayani Nachingwea kwa kudaiwa kukanyagwa na tembo, Serikali imesema itatumia helikopta kuwafukuza wanyama hao.

Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Kijiji cha Narungombe, Ramadhani Omari amethibitisha kutokea tukio hilo.

Mwenyekiti huyo amesema Kuleni alikuwa ni Mkazi wa kijiji cha Likwela ambaye huenda katika Kijiji cha Narungombe kwenye shughuli za kilimo.

“Nimepata taarifa ya tukio hilo kupitia kwa mtu mmoja aliyenipigia simu na nilipo fika kwenye eneo la tukio nimeukuta mwili wa marehemu amepondwa pondwa na umeshaanza kuharibika,” amesema Omari.

Mwenyekiti ameongeza kwa kusema hali ya usalama kijijini kwake siyo mzuri kufatia tembo kuzurula kijijini hapo na kusema kuna wakati wanafika hadi majumbani.

“Tumetoa taarifa kwa askari wa wanyamapori hawajatupa ushirikiano labda kwa tukio hili la mtu kufariki wana weza wakafika,” amesema.

Shuhuda wa tukio hilo Mustafa Abdallah    amesema alipita siku ya Agosti 11 saa kumi alasiri akielekea shambani kwake na kuikuta baiskeli ya marehemu imeegeshwa njiani.

“Jana (Agosti 13) nikiwa narudi kutoka shambani nilipofika eneo hilo nikaikuta baiskeli bado imeegeshwa eneo lilelile nikiangalia chini nikakuta nyayo za tembo nikaanza kutafuta ndipo nilipo uona mwili wa marehemu. Nikatoa taarifa kwa uongozi wa kijiji,” amesema mkazi wa eneo hilo Mustafa Abdallah.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mwananchi kuuwawa na tembo.

Moyo amesema kutokana na kuendelea kwa matukio ya tembo kufanya uharibifu wa mazao na wakati mwingine kusababisha vifo.

Hivyo serikali imelazimika kupeleka helikopta itakayosaidia kuwarudisha tembo hao hifadhini.

Leave a Reply