• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Waziri Ummy aunda kamati ya kuchunguza malalamiko ya madaktari wa Interns

Bynijuzetz

Aug 14, 2023

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya imepokea nakala ya barua ya wazi tarehe 21.07.2023 iliyoandikwa na Wawakilishi wa Madaktari waliohitimu mafunzo ya utarajali (Interns), iliyoelekezwa kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa imeainisha hoja kadhaa zinazohusu malalamiko juu ya mitihani ya usajili kabla na baada ya utarajali inayotolewa na Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT).

Waziri Ummy Mwalimu amesema kufuatia malalamiko hayo ameamua kuunda Kamati huru ya uchunguzi yenye Wajumbe 13 ikiongozwa na Prof. Muhammad Bakari (Mganga Mkuu wa Serikali Mstaafu) ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ambapo Kamati hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufuata hadidu za rejea zilizoainishwa na Wizara ili kuchunguza msingi wa malalamiko yaliyotolewa na Madaktari tarajali katika barua yao na itatoa mapendekezo yatakayopelekea kutatuliwa kwa changamoto zitakazobainika.

“Katika muda wote ambao Kamati itakuwa inatekeleza majukumu yake, taratibu nyingine za mafunzo ya watarajali zitakuwa zinaendelea kama ilivyoainishwa kwenye sheria, Watarajali wenye changamoto tofauti na hii au inayoendana na hii tunawashauri wawasilishe changamoto hizo kwa Baraza la Madaktari ili kupata msaada zaidi”amefafanua Ummy Mwalimu

Nihitimishe kwa kuwasihi Madaktari tarajali wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Kamati itakua inafanya uchunguzi na pale watakapohitajika kutoa maelezo mbele ya Kamati watoe ushirikiano unaostahili, aidha niwahakikishie kuwa, Wizara itasimamia haki na ustawi wa taaluma ya Madaktari nchini”

Leave a Reply