• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

TLS wampongeza Rais Samia kwa Uongozi na Utawala bora

Bynijuzetz

Aug 15, 2023

Wakati kila mtu. akiwa na mtazamo wake juu ya vinavyoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu serikali, Uongozi wa Tanganyika Law Society (TLS) kupitia Rais wake Wakili Harlod Sungusia umeamua kutoa maua ya pongezi kwa Rais Samia juu ya Yawala bora.

Mhe. Rais Suluhu Samia tunakushukuru sana kwa uongozi wako bora uliojaa utu utawala bora, malengo mema na bora kabisa ya kujenga maridhiano na kuleta maridhiano ya mifumo, sera na sheria na kutekeleza mipango yakujenga Taifa letu kuwa bora na imara kiuchumi na kijamii”…

Tanganyika Law Society tunatambua juhudi zako kubwa za kuwakaribisha wadau wa maendeleo nchini kuvutia mitaji na wawekezaji pamoja na kuongeza fursa za ajira, kuimarisha huduma za jamii hususani elimu, afya, maji na kwa kweli ni vigumu kwa muda huu mfupi kutaja mambo haya makubwa Mhe. Rais umeyafanya kwetu kwa kipindi hiki kifupi, tunaamini kwamba kwa mwendo huu uchumi wetu wa Taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja bila shaka utaendelea kuwa bora zaidi Tunakushukuru sana Mhe. Rais” Wakili Harlod Sungusia.

Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika Tanganyika Law ameyazungumza hayo jana ikulu ya Chamwino baada ya uongozi wa chama hicho na Zanzibar Law Society(ZLS) kukutana na Mhe.Rais Samia.

Leave a Reply