• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Wakili Philip akerwa na Jeshi la Polisi kumzuia kuonana na wateja wake amabao ni Wakili Mwambukusi na Mdude Nyagali

Bynijuzetz

Aug 15, 2023

Wakili Philip Mwakilima anayemwakilisha Boniface Mwabukusi kwenye kesi zinazomkabili, ameeleza kukerwa na kitendo cha jeshi la polisi kumzuia kuonana na wateja wake (Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali) wakati anaruhusiwa kisheria. Wakili Mwakilima amesema tangu wateja wao wakamatwe hadi leo Jumanne bado hawajapelekwa mahakamani jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Kitu cha kusikitisha ambacho nimekuwa nakipata kutoka kwa Jeshi la Polisi ni manyanyaso dhidi yangu, nashangaa, sheria inaniruhusu mimi kuonana na mteja wangu (Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali) nikiwa na askari anayekuwa zamu kwa wakati huo lakini nimezuiliwa na cha kushangaza wengine wanaruhusiwa”,

Kitendo kinachofanyika si haki kabisa kwa sababu mimi naruhusiwa kisheria.

Leave a Reply