• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Prof. Kitila Mkumbo akaa mezani na Balozi wa Marekani nchini kujadili mahusiano ya Kiuchumi

Bynijuzetz

Aug 16, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amefanya mazungumzo na Mhe. Michael Battle, Balozi wa Marekani nchini, jana tarehe 15 Agosti, 2023 jijini Dodoma.

Viongozi hao wamejadiliana kuhusu namna ya kukuza uhusiano na ushirikiano wa uandaaji na utekelezaji wa mipango ya kiuchumi pamoja na kukuza uwekezaji baina ya Marekani na Tanzania.

Aidha, wamekubaliana kuharakisha ukamilishaji wa Jukwaa la Majadiliano (Commercial Dialogue) baina ya Marekani na Tanzania ambalo litakuwa nguzo muhimu ya kuhamasisha Biashara na fursa za uwekezaji.

Mhe. Waziri Mkumbo amemuhakikishia Balozi kuwa ,Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini ili kukuza biashara na uwekezaji na amempongeza Mhe. Balozi kwa kuwa balozi mzuri wa kuitangaza vema Tanzania.

Leave a Reply