• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mwanaume mmoja afariki kwa ajali ya gari huku mwingine akiokolewa

Bynijuzetz

Aug 23, 2023

Mwanaume mmoja Abdallah Jafari (27) ambaye alikuwa amebanwa kwenye gari kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Miono Wilayani Chalinze Mkoani Pwani amefariki dunia huku mwenzake Mbwana Said (37) ambaye alikuwa Dereva wa gari hilo akiokolewa akiwa hai.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani Jenifa Shirima amesema Mbwana ambaye alikuwa Dereva wa Gari hilo ameokolewa baada ya Askari wa kikosi cha zimamoto na Uokoaji kufika eneo la tukio huku wakitumia vifaa vya kisasa vilivyopo kwenye gari yao mpya na kufanikiwa kutengeneza nafasi na kisha kuwatoa yeye na Abdallah (Utingo wa gari) ambapo walipofikishwa Hospitali ilibainika Jafari amefariki .

Kamanda Jenifa amesema katika kuhakikisha kazi za uokoaji zinafanyika kwa ufanisi tayari Serikali imelipatia Jeshi la Zimamoto gari mbili mpya za kisasa zenye vifaa maalumu vya uokoaji zinapotokea ajali barabarani huku akitoa wito kwa Wananchi kuwa panapotokea ajali au matukio kama hayo kuwasiliana na Jeshi hilo haraka kwa namba 114 ili wawahi kuokoa maisha ya Watu na mali.

Leave a Reply