• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Kwanini Mkutano wa Brics unaendelea bila Uwepo wa Putin

Bynijuzetz

Aug 24, 2023

Rais wa Russia, Vladimir Putin hajaweza kuhudhuriaa mkutano wa viongozi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya BRICS ana kwa ana, badala yake atahudhuria kwa njia ya mtandao.

Brics inaundwa na mataifa ya Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

Mtandao wa Time, umeandika kuwa; wakati viongozi wengine wa mataifa hayo watahudhuria mkutano huo, huku wengine wakiwasili jijini Johannesburg, Afrika Kusini; Rais Putin atashiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao (video conference).

Sababu ya kufanya hivyo inaelezwa ni kutokana na hati ya kukamatwa kwa Rais huyo, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC); ambayo kimsingi iliiweka Afrika Kusini (mwenyeji), kwenye wakati mgumu, hatimaye kusababisha Putin kubaki nyumbani.

Hiki ndicho kinafanyika wakati kundi hili la mataifa yanayoinukia kiuchumi, wanapofanya mkutano kwa siku tatu, ambao umeanza jana Jummane Agosti 22, 2023 katika jiji kubwa na kitovu cha kifedha nchini Afrika Kusini.

Putin kuhudhuria kwa njia ya mtandao

Kwa kawaida, viongozi wote kutoka nchi za Brics uhudhuria mikutano yake ya kilele, huku Rais wa China China Xi Jinping akitarajiwa pia kushiriki mkutano huo wa kwanza wa ana kwa ana wa umoja huo tangu janga la Uviko-19 litokee.

Hata hivyo, kushtakiwa kwa Putin na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Machi mwaka huu, akihusishwa na uhalifu wa kivita kuhusu kuondolewa kwa watoto kutoka Ukraine, kuliiacha Afrika Kusini na kitendawili kikubwa cha kidiplomasia.

Afrika Kusini na Russia zina uhusiano mkubwa na zina uhusiano wa karibu kihistoria, lakini Afrika Kusini pia imetia saini mkataba wa mahakama ya kimataifa. Hiyo ilimaanisha kuwa ingelazimika kumkamata Putin kwa waranti ya ICC ikiwa angekanyaga ardhi ya Afrika Kusini.

Afrika Kusini ilishawishi kwa miezi kadhaa kabla ya mkutano huo kumshawishi Putin kubaki nyumbani ili iweze kuepusha tatizo hilo, maafisa wa Afrika Kusini wamesema.

Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile alisema mwezi uliopita kwamba Putin alikuwa amedhamiria kufika kabla ya kutangazwa kwa makubaliano ya yeye kushiriki kwa njia mtandao

“Ni kama vile unamwalika rafiki yako nyumbani kwako, na kisha kuwakamata,” Mashatile alisema wakati huo. “Ndiyo maana kwetu kutokuja kwake ndio suluhisho bora. Warussia hawana furaha, ingawa. Wanataka aje,”

Ikulu ya Kremlin haikusema kama Putin alikuwa na nia ya kusafiri kwenda Afrika Kusini, lakini alisisitiza kuwa bado atachukua jukumu muhimu katika mkutano mkuu wa kilele leo ambapo atahutubia wajumbe kwa njia ya video.

“Tunazungumza juu ya ushiriki kamili,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema. “Hii itajumuisha hotuba ya rais na, ikibidi, kushiriki katika kubadilishana mawazo.”

Wengine wanaotafuta BRICS kubwa zaidi

Mjadala mkuu utakuwa juu ya kupanua kambi ya mataifa matano. China na Russia zinaunga mkono Brics kubwa na zinaonekana kusukuma hilo. Takriban nchi 12 zimetuma maombi ya kuwa wanachama wapya, zikiwemo Saudi Arabia, Iran, Argentina, Algeria, Misri, Ethiopia na Falme za Kiarabu.

Lakini Brics ni shirika lenye msingi wa maelewano, na wanachama wote watano lazima wakubaliane kuhusu kanuni ya upanuzi na vigezo vya wanachama wapya kabla ya kuamua ni nani atajiunga.

Brazil, India na Afrika Kusini zinaonekana kutopenda sana upanuzi, zikihofia sauti zao zinaweza kupunguzwa, lakini umoja huo unaendelea na viongozi hao watano wanatarajiwa kupitia mapendekezo ya vigezo vya upanuzi.

Ikiwa sera hiyo itaidhinishwa, Brics kubwa zaidi inaweza kuonekana kama fursa kwa China na Russia kupanua ushawishi wao.

Mahusiano na Magharibi

Upanuzi unaowezekana wa Brics unaonekana na baadhi ya watu kama sehemu ya juhudi za China na Russia za kukabiliana na kundi la mataifa saba makubwa ya viwanda na taasisi nyingine za kimataifa za magharibi.

Umoja huo unasisitiza kuwa mwelekeo wake sio dhidi ya magharibi lakini katika kuangalia masilahi ya ulimwengu unaoendelea.

Bado, Brics imekosoa waziwazi kile inachokiita utawala wa magharibi wa kimataifa na taasisi za kifedha kama Umoja wa Mataifa (UN), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB) kwa madhara kwa ulimwengu unaoendelea.

Benki mpya ya maendeleo ya jumuiya hiyo, ina sera iliyoelezwa ya kujaribu kuhimiza biashara zaidi ya sarafu za ndani na kuondokana na dola.

Pia imeelezwa kuwa, kwa upande mwingine, Brics imetoa nafasi kwa maafisa wa China na Russia wakati mwingine kulaumu mataifa ya magharibi.

Hata hivyo, Afrika Kusini, ambayo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Brics, imesema hiyo haimaanishi kuwa umoja huo unachukua mkondo dhidi ya nchi za magharibi chini ya ushawishi wa China na Urusi huku kukiwa na mvutano wa kijiografia wa magharibi-mashariki.

“Kuna simulizi ya bahati mbaya inayoendelezwa kwamba Brics inapinga Magharibi, kwamba Brics iliundwa kama ushindani kwa G-7 au ‘Global North,’ na hiyo si sahihi,” Anil Sooklal, Balozi wa Afrika Kusini katika Brics alisema. “Tunachofanya ni kutafuta kuendeleza ajenda ya Kusini (Global South).”

Leave a Reply