• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Jeshi la Niger limewataka mabalozi wa Magharibi pamoja na Marekani kuondoka nchini humo haraka

Bynijuzetz

Aug 26, 2023

Jeshi la Niger ambalo linaongoza Nchi hiyo baada ya kumpindua Rais limetoa saa 48 kwa Balozi wa Marekani nchini humo na Mabalozi wa Nchi nyingine nne za Ufaransa, Ujerumani , Ivory Coast na Nigeria kuondoka Niger.

Daiy Post iimeripoti kuwa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema sababu ya kuwatimua Mabalozi hao ni kutokana na msimamo wao wa kutoiunga mkono Niger na kutaka Rais aliyepinduliwa arejeshwe madarakani.

Sababu nyingine ni Wizara za Mambo ya Nje za Mataifa hayo ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa kukataa mwaliko wa Maafisa wake kukutana na Waziri mpya wa Mambo Nje wa Niger.

Leave a Reply