• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Serikali yatangaza kuendelea na mchakato wa uwekezaji bandarini kwa kushirikiana na DP World

Bynijuzetz

Aug 28, 2023

Kila hatua na kadri majadiliano yatakavyokuwa yanaendelea ikiwemo kuafikiana au kukubaliana pande zote kati ya Serikali ya Tanzania na mwekezaji kwenye uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam , umma wa Watanzania tumehakikishiwa kuwa utajulishwa.

Hayo yalisemwa Agosti 26, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna mkataba wowote wa utekelezaji kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa bandari ambao umeshasainiwa.

Msigwa amesema, baada ya hatua ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai hatua itakayofuata ni mikataba ya utekelezaji.

Kuhusu mikataba hiyo ya utekelezaji, Msigwa amesema

“Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani”

Msigwa ameendelea kwa kusema kuwa, hatua itakayofuata ni uandaaji wa nyaraka na katika hatua hii ndipo miradi ya utekelezaji itaandaliwa huku akiendelea kusisitiza kuwa hakuna bandari iliyouzwa.

Leave a Reply