• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Uteuzi wa Dotto Biteko ni Pasua kichwa kwa wadau wa siasa nchini.

Bynijuzetz

Aug 30, 2023

Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Suluhu Samia kuanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu na kumteua mbunge wa jimbo la Bukombe Mhe. Dkt.Dotto Biteko kushika nafasi hiyo umeibua mjadala mkubwa nchini Tanzania huku wadadisi na wachambuzi wa maswala ya kisiasa wakipokea uteuzi huo kwa hisia tofauti tofauti.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Anna Henga amesema, cheo cha Naibu Waziri Mkuu sio cheo cha kikatiba lakini katiba ya Tanzania ibara ya 36 imempa Rais mamlaka kuanzisha nafasi yoyote ile katika utumishi wa serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Duru zingine za kisiasa zinataja kitendo hicho cha kumteua Mhe.Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu kuwa ni kete mhimu ya awamu ya sita kujijenga kisiasa katika kanda ya ziwa yenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania huku ikitajwa ni eneo lenye kubeba wapiga kura wengi katika kipindi cha uchaguzi huku umakini na uchapakazi wa Dkt. Dotto Biteko ukitajwa kuongeza ufanisi ndani ya serikali.

Mbali na Mhe.Dotto Biteko kuteuliwa nafasi hiyo pia atakuwa na majukumu ya kuratibu shughuli za serikali huku akiiongoza pia wizara nyeti kabisa ya Nishati ambayo kwa siku za hivi karibuni imekumbwa na changamoto za ukosefu wa umeme wa uhakika.

Leave a Reply