• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Miaka 80 Jela kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali.

Bynijuzetz

Aug 31, 2023

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu Cyprian Kasuva kifungo cha miaka 80 jela kwa kosa la kukutwa na makosa matatu, kosa la kwanza kukutwa na nyara za Serikali (kichwa cha Tembo na meno yake), kosa la pili kukutwa na silaha (Magobore matatu) na kosa la tatu kukutwa na risasi 35.

Cyprian(44) Mkazi wa Kalenga Iringa Vijijini inadaiwa alitenda kosa hilo May 09, 2022 katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo akiwa anabanika nyama ya Tembo, Askari wa Wanyama Pori wakafanikiwa kumkamata.

Kosa la kukutwa na kichwa cha Tembo na meno yake hukumu yake ni kifungo cha miaka 30 au faini ya shilingi milioni 348, kosa la kukutwa silaha (Magobole matatu) hukumu yake ni kifungo miaka 25 na kukutwa na risasi 35 hukumu yake ni kifungo miaka 25 na hivyo kufanya jumla ya makosa yote kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 80 ( kuitumikia kwa pamoja).

Kesi hiyo imesomwa na Hakim Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa na ilikuwa na Mashahidi 6 huku ikisimamiwa na Mwendedha mashtaka wa Serikali Barton Mayage, Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Cyprian aliiomba kupunguziwa adhabu kwasababu ni kosa lake la Kwanza na ana Watoto watatu wanamtegemea lakini hata hivyo akahukumiwa miaka 80.

Leave a Reply