• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Tundu Lissu azungumzia kuvunjika kwa maridhiano kati ya CCM na CHADEMA

Bynijuzetz

Sep 2, 2023

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Tundu Lissu amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekataa kuendelea kwa maridhiano kwakuwa CHADEMA ilipeleka mapendekezo mazuri ya kila kitu kinachohitajika kufanyika, wakati, muhusika na ratiba ambayo wanaamini ingekuwa muongozo sahihi ambao ungepelekea kupatikana kwa Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 lakini mapendekezo yote yamekataliwa kwa maandishi.

Akizungumza kupitia jukwaa la mijadala la mitandao ya kijamii Lissu amesema imefikia miezi mitatu tangu mapendekezo hayo yakataliwe na hivyo mazungumzo ya mwisho yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2023 CHADEMA ilitoa msimamo kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yataendelea endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu atabadilisha msimamo wa chama chake kwenye jambo hilo.

Amesema haikuwa dhamira ya chama hicho kujiondoa kwenye mchakato huo lakini kitendo cha mapendekezo yao yote kukataliwa kimewaondolea imani dhidi ya kuendelea mjadala huo.

Ameendelea kudai kuwa kauli iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba hivi karibuni Dkt.Damasi Ndumbaro inadhihirisha msimamo ilionao CCM na Serikali

Leave a Reply