• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Teuzi za mama zazidi kumwangika kama njugu, Ashusha uteuzi usiku wa manane

Bynijuzetz

Sep 4, 2023

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Amemteua pia Balozi Said Shaib Mussa – Balozi wa Tanzania, Kuwait kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Fama Rajab ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, Qatar.

Amemteua pia Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Dkt. Evaristo Longopa ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Rais Samia amewateua pia wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Lameck Michael Mlacha, Jaji Paul Joel Ngwembe, Jaji Mustafa Kambona Ismail na Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa.

Rais amewateua pia wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, Dkt. Evaristo Longopa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Wilbert Martin Chuma, Sharmillah Sarwat, Arnold John Kirekiano, Martha Boniface Maze, Ferdinand Hilali Kiwonde, Said Rashid Ding’ohi, Dkt. Angelo Kataraiya, Sarah Duncan Mwaipopo na Ntuli Lutengano Mwakahesya.

Wengine walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ni Griffin Venance Mwakapeje, Dkt. Dafina Daniel Numbaro, Emmanuel Ludovick Kawishe, Abdallah Halfan Gonzi, Kamazima Kafanabo Idd , Frank Muoba Mirindo, Hadija Ally Kinyaka, Aisha Ally Sinde, Hussein Salum Mtembwa na Irene Daniel Musokwa.

Leave a Reply