• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mzee Kinana awaonya wanapambana kwa nia ya kuwania Ubunge uchaguzi ujao

Bynijuzetz

Sep 6, 2023

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua Wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani akisema wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, utaratibu na miongozo ya uchaguzi ndani ya CCM.

Kinana ameyasema hayo September 05, 2023, Wilayani Hai, Kilimanjaro katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Hai, uliohusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, Jimboni ambapo amesema watakaobainika wanajipitisha kusaka ubunge na udiwani hawatapitishwa na vikao vya maamuzi kugombea nafasi hizo hata kama wataongoza katika kura za maoni

“Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa”

“Hatuna nafasi ya kuhangaishwa na Watu wanaotafuta uongozi kipindi hiki, wasubiri hadi mwezi wa saba mwaka 2025, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itaamua tarehe ya kwenda kuchukua fomu, kabla ya hapo unavunja kanuni”

“Aliyeanza kampeni mapema, alitoa rushwa, alikivuruga Chama, hata upate kura za Wajumbe wote hutapita, je ulitoa rushwa, ulizingatia kanuni, uliwachafua Viongozi wenzako walioko madarakani? Kwa hiyo unaweza ukawa wa kwanza lakini ukawa wa mwisho”

Leave a Reply