• Tue. Feb 27th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Naibu Waziri Mkuu na Naibu waziri wa Nishati wapokelewa rasmi na menejimenti na watumishi wa Wizara

Bynijuzetz

Sep 6, 2023

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga Septemba 04, 2023 wamepokelewa rasmi na menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kushika nyadhifa hizo.

Akizungumza na Menejimenti na Watumishi hao tarehe 4 Septemba, 2023, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia kwa kumuamini katika kuisimamia sekta ya nishati na ameahidi kuwa yeye pamoja na naibu waziri watafanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kuitendea haki imani hiyo.

Leave a Reply