• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Jeshi la Polisi lazuia mikutano ya Chadema wilayani Ngorongoro

Bynijuzetz

Sep 7, 2023

Jeshi la Polisi Wilayani Ngorongoro limesitisha mikutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliyotarajiwa kufanyika septemba 8-9 mwaka huu maeneo ya kata 3 zilizopo tarafa ya Loliondo na kata 3 zilizopo tarafa za Ngorongoro kwa kile ilichodai kuingia na kutoka eneo hilo ni sharti kufuata taratibu zinazosimamia eneo hilo (kupata kibali kutoka Mamlaka ya Ngorongoro.

Aidha barua yakusitisha Mikutano hiyo imeeleza kuwa upande wa tarafa ya Loliondo kulingana na taarifa mbalimbali walizonazo kama jeshi la polisi haziruhusu kufanya shughuli za kisiasa hasa mikutano ya hadhara hadi wakati mwingine ambao utakuwa mwafaka kwa ustawi wa amani na utulivu wa wilaya hiyo.

Leave a Reply