• Tue. Feb 27th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Shambulio laua watu 16 Vita vya Ukraine

Bynijuzetz

Sep 7, 2023

Rais Zelensky amelaani shambulio la “makusudi” dhidi ya mji “wa amani” wa Ukraine wa Kostyantynivka.

Takribani watu 16, akiwemo mtoto, waliuawa katika mlipuko huo, ambao ulitokea kwenye mtaa wa soko lenye shughuli nyingi katikati ya siku, jambo ambalo ni la nadra.

Kostyantynivka, katika eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine, iko karibu na mstari wa mbele. Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha mlipuko mkali wa rangi ya machungwa mwishoni mwa barabara ambapo watu walikuwa wakifanya manunuzi.

Urusi bado haijasema lolote kuhusu shambulio hilo.

Bw Zelensky, ambaye ameilaumu Moscow, alisema waliouawa ni “watu ambao hawakufanya lolote baya” na kuonya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Takribani watu 28 wanadhaniwa kujeruhiwa. Soko, maduka na duka la dawa vyote vimeripotiwa kushambuliwa.

Polisi na wahudumu wa uokoaji wako kwenye eneo la tukio, wakiendelea kutafuta manusura.

Inaonekana kuwa shambulio baya zaidi la aina yake kwa miezi kadhaa

Leave a Reply