• Tue. Feb 27th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Moto Uliokuwa changamoto wadhibitiwa mlima Kilimanjaro

Bynijuzetz

Sep 13, 2023

Mamlaka nchini Tanzania imefanikiwa kuudhibiti moto uliozuka katika mlima Kilimanjaro huku zaidi ya ekari 2000 za uoto wa asili zikiwa zimeteketea na moto.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka za Hifadhi nchini humo, William Mwakilema aliiambia BBC kuwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kudhibiti moto huo uliozuka Septemba 03 mwaka huu katika eneo la Rongai wilayani Rombo.

Mwakilima alisema, “ Tumefanikiwa kudhibiti moto uliowaka mlima Kilimanjaro licha ya kuwa umeathiri asilimia 1.2 ya eneo la hifadhi ya mlima huo, sawa na hekari 2049…

“…bado chanzo cha moto hakijafahamika lakini tunaendelea kufuatilia huku vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikiendelea kuwepo kwenye eneo hilo ili kuhakikisha moto huo haufukuti tena,” alisema Mwakilema.

Mwaka jana moto kama huo ulizuka na katika kipindi cha mwezi mmojana kuteketeza maelfu ya hekari za hifadhi ya mlima huo mrefu zaidi Afrika huku ukiathri miundombinu mbalimbali ya mawasiliano sambamba mimea ya asili.

Leave a Reply