• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mwakinyo, “Mtoto wa Morogoro azidi kumuomba dua Mungu atasikia kilio chake”.

Bynijuzetz

Sep 14, 2023

Bondia maarufu nchini na mwenye mkwanja, Hassan Mwakinyo amemtaka ‘Mtoto’ wa Morogoro aendelee kumuomba pambano kwani kuna siku dua zake zitajibiwa.

Akiongea kwa mbwembwe Bondia huyo mweye rekodi Bora kabisa nchini, Mwakinyo amedai lazima ajipange kwakuwa halitakuwa pambano la ‘Pesa ya Madafu’ kwani halitamuongezea Rank.

”Sijaona mpinzani wangu, kwa sabau sina ninachokitaka kwanza kutoka kwao labda kama wao wanacho wanachokitaka kutoka kwangu, la pili ngumi ni mchezo ambao hautakiwi kumfagilia mtu, mpe mtu heshima lakini usiamini kama yeye ni bora kuliko wewe hicho kitu hakijaumbwa.”

”Tatu Boxer yoyote ambaye ana nia na mimi aendelee kuniomba kwa sababu hata huyu Mkenya alikuwa akiniimba sana lakini Mungu amejibu dua zake, kwa hiyo kuna siku pia huyu Mtoto wa Morogoro dua yake itajibiwa aendelee tu kuvuta subra na watu wa Morogoro waendelee kumswalia Mtume sana. Sio jambo kubwa kwa sababu sio maajabu ni kiasi cha kuamka tu nina akili mbaya nikaamua.”

”Sema tu wajiandae kwa sababu haiwezi kuwa pesa ya madafu, sabau sio kitu ambacho kitaninufaisha kama mchezaji, sitaweza kupata rank ya maana lakini wafanyaji kwao itakuwa ni historia kwa sababu ni kitu ambacho kitawapa wao hela zaidi na sisi inabidi tupate hela ili baada ya pambano iwepo alama kwamba zile ni ‘apartment’ za Mwakinyo alipigana na mtu fulani ndiyo baadaye akawekeza pale.”

Leave a Reply