• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Vifo vilivyosababishwa na mafuriko vyapelekea kukamatwa kwa Meya nchini Libya

Bynijuzetz

Sep 26, 2023

Meya wa mji wa Libya wa Derna ulioharibiwa na mafuriko makubwa amekamatwa kuhusiana na maafa hayo, maafisa wanasema.

Abdulmenam al-Ghaithi alikuwa miongoni mwa maafisa kadhaa walioshtakiwa kuhusiana na maafa yaliyowaua maelfu ya watu mashariki mwa Libya mapema mwezi huu.

Wiki iliyopita, wakazi wa Derna wenye hasira waliichoma moto nyumba ya meya wakimpinga

Ofisi ya mwanasheria mkuu, iliyoko katika mji mkuu wa Tripoli, ilisema Jumatatu kwamba maafisa hao “wanawajibika kwa kusimamia vifaa vya mabwawa ya nchi” na kwa hivyo imefungua kesi ya jinai dhidi yao.

Baadhi ya maafisa hao akiwemo Bw al-Ghaithi tayari wamezuiliwa kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, ofisi ya mwanasheria mkuu iliwashutumu maafisa hao kwa makosa mengi, kama vile usimamizi mbaya wa fedha zilizokusudiwa kutunza mabwawa yaliyopasuka na kusababisha mafuriko huko Derna.

Ofisi yake pia ilisema kuwa maafisa hao wameonyesha kutojali kwa kushindwa kuchukua tahadhari, na kusababisha vifo vinavyotokana na mafuriko na hasara ya kiuchumi kwa Libya.

Bw al-Ghaithi amezidi kushutumiwa kwa kutumia mamlaka yake vibaya.

Libya imegawanywa katika tawala mbili pinzani – moja mashariki na moja magharibi. Kwa vile mwanasheria mkuu yuko Tripoli, magharibi, haijabainika ni kwa kiwango gani anaweza kuamuru kukamatwa kwa watu mashariki.

Siku ya Jumapili, serikali ya mashariki ilisema kwamba idadi ya vifo vilivyothibitishwa kutokana na mafuriko imefikia 3,868.

Ofisi ya mwanasheria mkuu ilisema kuwa uchunguzi kuhusu maafisa wengine unaendelea na kunaweza kuwa na watu wengine waliokamatwa.

Leave a Reply