• Fri. Feb 23rd, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Baada ya kuapishwa, Mkurugenzi wa Tanesco apewa miezi sita suala la umeme kukatika

Bynijuzetz

Sep 27, 2023

Rais Samia ampa miezi sita Mkurugenzi Tanesco, asisikie tena kelele za kukatika kwa umeme

Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi mpya wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Gissima Nyamo- Hanga kuhakikisha anasimamia ukarabati wa mitambo na kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme kwa muda wa miezi sita.

Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliyowateua Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Mkurugenzi mpya wa Tanesco siyo mgeni, nenda kaanzie pale Maharage alipofikia, najua utaweza, nakupa miezi sita nakuangalia, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa mitambo ya umeme, baada ya miezi sita nisisikie tena kelele za kukatika kwa umeme,” amesema Rais Samia.

Leave a Reply