• Tue. Feb 27th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Byabato awataka watendaji kanda ya Ziwa kuhakikisha miradi inasimamiwa kwa kasi na ufanisi

Bynijuzetz

Sep 27, 2023

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Stephen Byabato, amewataka watendaji na wasimamizi wanaosimamia utekelezaji wa Programu na miradi mbalimbali katika Jiji la Mwanza, kupitia Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, kuhakikisha inatelezwa kwa kasi na ufanisi ili iwanufaishe wananchi wenye uhitaji.

“Nitoe rai kwenu watendaji na wasimamizi wote wa miradi hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inayotekelezwa katika Kanda ya Ziwa kupitia LVBC, kuhakikisha sote kwa umoja wetu tunafanya kazi usiku na mchana kutimiza adhma ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ya kuona Wananchi wa Tanzania, wananufaika moja kwa moja na fursa zinazotokana na Jumuiya kijamii na kiuchumi”.Amesema Mhe.Byabato.

Leave a Reply