• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Klabu ya mpira ya KMC imepewa Onyo kali na bodi kuu Tanzania

Bynijuzetz

Sep 28, 2023

Klabu ya KMC imepewa Onyo Kali na bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) kwa kosa la kuwakilishwa na maafisa wanne tu badala ya watano kwenye mkutano wa maandalizi ya dhidi ya JKT Tanzania uliofanyika Septamba 15, 2023 uliomalizika Kwa ushindi wa 2-1 kwa KMC.

Aidha KMC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kocha wake mkuu, Abdihamid Moalin na mchezaji Waziri Junior kuchelewa kufika kwenye mkutano wa Wanahabari Septemba 14, 2023.

Wawili hao walifika mkutanoni saa 5:18 asubuhi badala ya saa 5:00 asubuhi kwa mujibu wa ratiba ya mikutano hiyo ya kikanuni.

Leave a Reply