• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Viongozi wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania wamekutana na Naibu Msimizi mkuu wa USAID

Bynijuzetz

Sep 28, 2023

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe.Nassor Mazrui (Mb) na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr John Jingu, na Dkt Atul Gawande, Naibu Msimamizi Mkuu wa shirika la USAID wamekutana Atlanta, Marekani na kujadili ushirikiano katika kutekeleza vipaumbele vya sekta ya Afya.

Viongozi hao waliishukuru USAID kwa kuchangia uanzishwaji wa Mfumo wa Huduma ya Usafirishaji wa dharura kwa mama wajawazito na waliojifungua na watoto wachanga ambao hadi hivi sasa unatekelezwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao walikubaliana kushirikiana katika utekelezaji wa Program mpya ya Watumishi wa Afya Ngazi ya jamii ambao unatarajiwa kuzinduliwa kwa pande zote mbili za Muungano.

Leave a Reply