• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Mlipuko wauwa watu zaidi ya 50 nchini Pakistan wakiwa kwenye sherehe za Maulid

Bynijuzetz

Sep 29, 2023

Takriban watu 50 wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea Pakistan, polisi wameiambia BBC.

Mlipuko huo ulitokea karibu na msikiti mmoja katika mkoa wa kusini magharibi wa Balochistan siku ya Ijumaa wakati watu walipokusanyika kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.

Polisi wanashuku lilikuwa shambulio la kujitoa mhanga lililolengwa katika mkusanyiko wa kidini katika mji wa Mastung.

Maafisa wametangaza hali ya hatari.

Majeruhi wanasafirishwa hadi hospitali mbili, polisi wamesema.

Maafisa wawili wa polisi wa mji wa Mastung walithibitisha hesabu ya vifo kwa BBC News.

Waziri wa Mambo ya Ndani Sarfraz Bugti aliutaja mlipuko huo kuwa “kitendo cha kuchukiza sana”.

Video nyingi kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha majeruhi wakiokolewa na wahudumu wa dharura na wenyeji.

Hadi kufikia sasa, hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Leave a Reply