• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Tembo aliyepotea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo auawa

Bynijuzetz

Oct 10, 2023

Tembo aliyetoroka kutoka mbuga ya wanyama ya Virunga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameliwa na wakazi wa kijiji jirani.

“Ni kama bahati ilianguka kutoka mbinguni kwa ajili yetu,” kikundi cha wahifadhi kilinukuu watu “walioshangilia” kutoka kijiji cha Katwiguru wakisema.

Shirika lisilo la kiserikali, ambalo linafanya kazi na mamlaka ya wanyamapori ya nchi hiyo Congolese Institute for the Conservation of Nature(ICCN), lilituma ujumbe kwenye mtandao wa X, zamani ikifahamika kama Twitter kwamba haijabainika ikiwa ni waasi au wanakijiji waliomuua mnyama huyo.

Uzio wa umeme unachozunguka mbuga hiyo wiki kadhaa zilizopita uliharibiwa na “vijana” kuwaruhusu tembo wawili kupotea siku ya Jumatatu, shirika la habari la AFP linaripoti ICCN.

Hatima ya tembo wa pili haijulikani. Virunga ni mbuga maarufu ya wanyamapori katikati ya eneo linalokabiliwa na mapigano ambapo vikundi kadhaa vya wanamgambo vinafanya kazi karibu na mpaka wa Rwanda na Uganda.

Juhudi za uhifadhi zimesababisha vikosi vya waasi kutoka katika mbuga hiyo – ambayo ina urefu wa kilomita za mraba 7,800 (maili za mraba 3,000) – na kuunda eneo salama kwa tembo.

Kulingana na tovuti ya mbuga hiyo, tembo 580 walihamia kwenye mbuga hiyo mnamo 2020 na kuunda kundi la takriban 700.

Leave a Reply