• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Benki ya NMB yatangaza mafanikio ya kifedha kwa kipindi cha mwezi Septemba

Bynijuzetz

Nov 1, 2023

Benki ya NMB imetangaza kupata matokeo imara ya kifedha katika kipindi kilichoishia September 30 mwaka 2023, ambapo faida kabla ya kodi ya Benki imefikia Tsh. bilioni 569 ikiwa ni ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na Tsh. bilioni 464 za kipindi kama hicho mwaka jana.

Faida baada ya kodi ya Benki hii kiongozi nchini imeongezeka kwa asilimia 22 na kufikia Tsh. bilioni 398 ukilinganisha na Tsh. bilioni 324 zilizopatikana kipindi kilichoishia September 2022.

NMB imesema ufanisi huu mkubwa ni mwendelezo wa utekelezaji makini wa Mkakati wa Benki na nidhamu kubwa ya utekelezaji wa Mkakati huo, ambapo matokeo yake ni ukuaji wa biashara, nidhamu yaudhibiti wa gharama za uendeshaji na usimamizi mzuri wa ukopeshaji, ukuaji huu mkubwa wa biashara pia, ni matokeo ya utulivu na mazingira wezeshi ya kibiashara na kiutendaji nchini.

“Benki imeendeleza ufanisi wa mapato ambapo mapato halisi ya riba yameongezeka kwa asilimia 20 hadi kufikia Bilioni 692, hasa kutokana na kuongezeka kwa mikopo kwa wateja binafsi na wale wakubwa, mapato yasiyotokana na riba nayo yameongezeka hadi kufikia TZS bilioni 334 ikilinganishwa na TZS bilioni 297 za mwaka 2022 ambalo ni ongezeko la asilimia 12”

Leave a Reply