• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Hukumu ya miaka 22 kwa aliyekamatwa na vipande 12 vya nyama ya swala Ikemewe.

Bynijuzetz

Nov 8, 2023

Mambo ya kufikiria kwenye hii hukumu;
1. Hivi ni kweli waongozaji wa hii kesi walikosa utu kiasi cha kutokutambua thamani ya mwanamke huyu mpambanaji ambaye hata kwa kumtazama tu unagundua hali yake ya kiuchumi?
2. Thamani ya haki kwa mtanzania iko wapi juu ya hukumu za kifedhuli kwa walipa kodi ikiwa hawaoni ubadhirifu mkubwa wa mabilioni ila uhujumu wa msakatonge kwa vipande 12 vya nyama ya swala?
3. Je, ni kweli wahujumu Uchumi na wezi wa fedha za Umma hawajaonekana au hawatambuliki kwa kubakisha kelele kama mbwa wabwekao bila meno wakati kodi za watanzania zikitafunwa na wapenda shibe wachache ili hali wenye nchi yao wakinyanyasika?

Unanafunga mtu miaka 22 kwa sababu umemkuta na kilo kadhaa za nyama pori. Wakati huo huo, mzungu analipia kibali cha TZS 5,000 kuua mnyama huyo huyo! Halafu mnaita NYARA ZA SERIKALI! Unagawa nyara ya Serikali kwa elfu 5 una akili wewe?

Hizi sheria ziliwekwa na wakoloni ili kuzuia wazawa wasifaidike na wanyamapori (rasilimali) zao, wakidhani kwamba wanyama watapungua. Wakati huo huo wanawasafirisha kwenda kwao. Wakoloni waliweka sheria hizi kali wakati wanaishi hapa Tanganyika.

Leo, wamerudi wanawadanganya na vipande vya fedha mnawaruhusu kuua wanyamapori, tena wanawaua kama sehemu ya MCHEZO (trophy hunting), kwa kibali elfu 5, halafu mnajiita mna akili timamu.
Baadhi ya washika mamlaka pia wamekuwa vibaraka juu ya uhujumu huu wakiwa hawachukuliwi hatua zozote za kisheria, mana wamekuwa wakijinufaisha wao kwamabilioni ya fedha na wasichukuliwe hatua.

Hatuna haja ya kutafuta ushahidi wa hili ikiwa bunge lenyewe linathibitisha uhujumu na wizi wa wenye mamlaka na wasichukuliwe hatua zozote kisheria ila mama huyu mwenye vipande 12 vya nyama pori,

Huu ni uonevu uliovuka mipaka japo hatuwezi kuingilia maamuzi ya mahakama ila jambo hili ni fedheha kwa mtanzania anayelipa kodi inayochangia kulipa mishahara inayofanya watoa hukumu wapate jeuri ya kuhukumu.

You’re bunch of IDIOTS!!

Leave a Reply