• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Watanzania wanaoshikiliwa mateka na kundi la Hamas wafanyiwa jitihada za kukombolewa kiusalama

Bynijuzetz

Nov 8, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen ameahidi dhamira yake binafsi ya kuimarisha juhudi za serikali ya Israel kuwatafuta wanafunzi wa Kitanzania Clemence Mtenga na Joshua Mollel ambao wameshikiliwa mateka na wanamgambo wa Hamas tangu Oktoba 07.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwenye mtandao wa ‘x’, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, January Makamba alisema amezungumza na waziri huyo kuhusu jitihada za kuwapata wanafunzi hao wawili, pamoja na mtazamo wa Israel kuhusu mzozo unaoendelea.

Bw Makamba amesema alisisitiza msimamo wa Tanzania kuhusu mzozo unaoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas wa Palestina.

Aliongeza, kunapaswa kuzingatiwa sheria ya kimataifa ya kibinadamu hasa ulinzi wa maisha ya raia.

Bw Makamba pia alishauri kuwa wanapaswa kusitisha operesheni za kijeshi ili kuruhusu juhudi za kibinadamu kuendelea pamoja na kurejesha mchakato wa amani.

Clemence na Joshua ni miongoni mwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas kwa karibu mwezi mmoja sasa.

Wawili hao walikuwa Kusini mwa Israel kuhudhuria programu ya mafunzo yanayohusiana na kilimo

Leave a Reply