• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Naibu Waziri wa Uchukuzi apeleka neema ya vifaa vya Hospitali Mufindi

Bynijuzetz

Dec 16, 2023

Mbunge wa Mufindi Kusini ambeye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amekabidhi kontena lenye shehene yenye vifaa mbalimbali vya Hospitali ya Wilaya ya Mufindi vyenye thamani ya Tsh. bilioni 1.8 leo December 16,2023, vifaa hivyo ni misaada aliyoitafuta yeye mwenyewe kutoka nje ya Nchi.

Kihenzile amegawa pia baiskeli kwa Watu wenye mahitaji maalumu katika Jimbo la Mufindi kusini na mitungi ya gesi kwa vikundi vya Mama lishe, mashine ya uzalishaji wa  vifaranga zenye thamani ya Tsh. milioni 10, mashine ya kufyetulia matofali yenye thamani ya milioni 15 na amekabidhi pia vyerehani 10 vya kushonea kwa vikundi vya Wanawake pamoja na pikipiki 16 kwa kila Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Mufindi Kusini.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Wahusika na Mgeni rasmi kwenye hafla ya uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2023  Issa Gavu,  katika Mkutano  Mkuu wa Jimbo la Mufindi kusini uliofanyika leo katika viwanja vya Mbalamaziwa, vifaa hivyo vimewasili nchini wiki hii kutoka nje ya Nchi.

Katika hatua nyingine Wajumbe wa Mufindi kusini wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mbunge wao huyo kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na wamemshukuru Rais pia kwa kuidhinisha fedha za miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika jimbo la Mufindi Kusini.

Leave a Reply