• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Niger, Mali na BUrkina Faso kung’atuka ECOWAS mara moja

Bynijuzetz

Jan 29, 2024

Serikali za kijeshi za Niger, Mali na Burkina Faso zimetangaza kujiondoa mara moja kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

Viongozi wa mataifa hayo matatu (3) ya ukanda wa Sahel wametoa taarifa yao ya pamoja jioni ya Jumapili, Januari 28.2024 ambapo pamoja na mambo mengine wamesisitiza kuwa uamuzi walioufanya ni huru na kwamba wameona sasa ni wakati muafaka wa kujiondoa katika jumuiya hiyo badala ya kuendelea kusubiri.

Katika taarifa hiyo msemaji wa jeshi la Niger Kanali Amadou Abdramane amesema jumuiya ya ECOWAS imeshindwa kuyasaidia mataifa hayo katika mapambano yao dhidi ya ugaidi na ukosefu wa usalama.

Aidha taarifa hiyo imeishutumu ECOWAS kwamba iko chini ya ushawishi wa mataifa ya kigeni, kusaliti misingi ya kuanzishwa kwake, na kuwa imekuwa tishio kwa wanachama wake na watu wake ambao inapaswa kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Itakumbukwa kuwa Niger, Mali na Burkina Faso zilisimamishwa uanachama na jumuiya hiyo huku Niger na Mali zikikabiliwa na vikwazo vikali.

Leave a Reply