• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

“Ningekuwa Rais”, Hatua kali kwa Jerry Silaa zingechukuliwa.

Bynijuzetz

Jan 29, 2024

Septemba 04, mwaka jana, Jerry Silaa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliwasili ofisi ya Wizara ya Ardhi jijini Dodoma na kukutana na watumishi wa wizara hiyo na katika mazungumzo yake na watumishi hao.

Waziri Silaa alitaja vipaumbele vyake 12, mbali na vile vya wizara ya ardhi ambalo ni jambo jema kwa mtu yeyote anaayetaka kufanikiwa katika utendaji wake.

Mara baada ya kutaja vipaumbele hivyo Waziri Silaa akageukia tahadhari ya rushwa kwa kujua kuwa moja ya maeneo yanayogubikwa kwa rushwa katika nchi hii ni eneo la ardhi.

Eneo hili la rushwa ndipo nilipoanza kupatwa na wasiwasi juu yake pale alipoeleza na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya Habari ikiwemo blogu maarufu ya Millard Ayo akisema kuwa “ Kuhusu rushwa sichukui rushwa, usiniletee hela, nitakuitia TAKUKURU, sina wakala, situmi sms, siuzi appointment, Dar niingilie upande wa wananchi”.

Katika nukuu hizo Waziri Jerry akaendelea kusema “Hakuna anayenimudu, Ilala nilikataa rushwa ya shilingi bilioni 1, tukatoa mapato bilioni 9- bilioni 32 -bilioni 54, tukakusanya data, leo miaka 9 ndio Satura (mkurugenzi) anakusanya data, ingawa gharama yake ni kubwa mkurugenzi wangu alisimamishwa kazi, afisa ushirika alipigwa risasi akaibiwa laptop tu”.

Likiwa hilo halijatulia Waziri Jerry Silaa akiwa mkoani Kilimanjaro Septemba 5 katika wilaya ya Moshi, alikutana na wataalamu wa ardhi katika moja ya ziara yake, ya kukagua ujenzi wa vituo vya mafuta, huko inaelezwa aliagiza ujenzi wa kituo cha mafuta cha mfanyabiashara Ibrahim Shayo usitishwe hadi wizara itakapotoa maelekezo mengine juu ya ujenzi wa kituo hiko.

Ingawa nyaraka za mfanyabiashara huyo zilionesha kuwa alifuata taratibu zote za ujenzi wa kituo hiko Waziri Silaa, aliwalaumu wataalam wa ardhi kuwa anajua michezo yao kujipigia pasi kwa mbele na kwenda kuiwahi akimaanisha kuwa wanatengeneza mazingiraam ya kunufaika binafsi kutokana na kanuni walizojiwekea.

Disemba 23, mwaka jana Waziri Silaa katika muendelezo wake wa kuzua sintofahamu, akiwa katika ukaguzi wa moja yaa vituo vya mafuta maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam,aliufahaamisha umma kupitia vyombo vya habaari vilivyokuwa hapo kuwa, alitengewa kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kupindisha utaratibu na fedha hizo alibainisha kuwa hazijaamfikia, ingawa waliompa taarifa juu ya uwepo wa mgao huo ni watu wake wa karibu wanaommudu.

Kwamba kuna mpango wa kupewa hongo na kwa kuwa, wahusika ni jamaa zake wanaofahamiana basi suala hilo likaishia kwa yeye kukataa kuchukua mgao lakini akaashindwa kuwaripoti katika mamlaka zinazozuia na kupambana na rushwa hii ni ajabu kubwa kwa mtu aliyesoma sheria na mwenye dhamana ya kiserikali kusimamia uadilifu.

Baada ya kauli hiyo ya Jery Silaa nilijipa kazi ya kufuatilia rekodi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kama alishawahi kuripoti katika mamlaka zinazoshughulikia rushwa juu ya yeye kutaka kupewa kiasi hicho cha fedha na zililenga kupitisha jambo gani katika mkasa ule wa kukataa shilingi bilioni moja akiwa meya wa Ilala?

Pia nikajiuliza je baada ya kukataa rushwa hiyo ya shilingi bilioni moja ambazo hajasema zililenga kumshawishi afanye nini je hiko kilichosababisha atake kupewa rushwa akiwa meya wa Ilala kilifanyika kwa muundo gani na kwa uhakika upi? Kunaweza kuwa na tafsiri nyingi juu ya kauli ya Silaa kukataa rushwa ya shilingi bilioni moja na kukaa kimya bila kuwafikisha wahongaji kwenye vyombo vya dola kwamba ililenga kutaka kiwango kiongezeke ama vinginevyo.

Lakini Jerry Silaa ameongeza kuwa baada ya kukataa kiasi hiko cha shilingi bilioni moja walifanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 9 hadi 32 na hatimaye 54 “Tukatoa mapato bilioni 9- bilioni 32 -bilioni 54, tukakusanya data, leo miaka 9 ndio Satura anakusanya data, ingawa gharama yake ni kubwa mkurugenzi wangu alisimamishwa kazi, afisa ushirika alipigwa risasi akaibiwa laptop”;alinikuliwa Waziri Silaa katika kikao hicho na watumishi wa Wizara ya Ardhi.

Hapa bado kuna utata mwingine kwamba alipokataa rushwa hiyo ambayo hakuitolea taarifa popote walilipa gharama kubwa ikiwemo mkurugenzi wake kusimamishwa kazi, Afisa Ushirika alipigwa risasi na kisha laptop pekee kuibiwa kwamba Jery alikuwa anawajua waliotaka kumhonga, akakaa kimya hakujishughulisha kuwafikisha katika vyombo vya dola akiwa kiongozi mwenye dhamana,lakini ukimya wake ukazaa uhalifu kwa Afisa Ushirika wake kupigwa risasi na kuibwa kwa laptop napo pia hakuona sababu yoyote ya kutoa taaarifa, hadi miaka 9 imetimia leo akiwa waziri ndiyo anaenda kuwaambia watumishi wa wizara tena mbele ya vyombo ya habari.

Katika mtazamo wa kawaida kauli zote tatu za Jeri Silaa aliyotoa akiwa Dodoma Septemba 4 ile ya utaalam wa kujitangulizia pasi akiwa mkoani Kilimanjaro na ile ya mwezi Desemba mwaka jana (2023) akiwa Mikocheni jijini Dar es Salaam zilipaswa kumuweka nje ya viongozi waadilifu na mamlaka za kiserikali zenye dhamana ya uchunguzi ziwe zinamchunguza Lakini pia hatua ya pili ya kauli yake inaweza kuwaogopesha wawekezaji wa ndani na nje ikiwa tu hawataelewa madhumuni ya Waziri silaa kujipigia pasi mbele na hivyo kuhatarisha jitihada zote za Rais kuwataka watanzania walio ndani na nje ya nchi kuwekeza nchini.

Ndiyo maana nikasema ningekuwa Rais ningemkabidhi Jerry Slaa mikononi mwa TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa).

Credits (John Marwa)

Leave a Reply