• Mon. Feb 26th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Kesi ya mwanamke aliyehukumiwa miaka 22 kisa nyama ya swala rufaa yaanza kusikilizwa Iringa

Bynijuzetz

Feb 2, 2024

Mahakama Kuu ya Mkoa wa Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Elvin Mgetta imesikiliza kesi ya rufaa namba 84101/2023 dhidi ya Jamhuri ya Mkazi wa Mtaa wa Isakalilo Manispaa ya Iringa ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala.

Akiongoza Jopo la Mawakili kwa kushirikana na Mwanasheria wa UWT kwa upande wa Mrufani,
Wakili Moses Abwindile amesema waliwasilisha sababu za rufaa 14 zilizowafanya wafikie hatua hiyo ambapo miongoni mwa hoja zilizowasilishwa ni kwamba Mkata rufaa hakutendewa haki ya kupewa msaada wa kisheria hasa kutokana na hali yake ya kiuchumi ambapo inadaiwa Mahakama ilipaswa kuwasiliana na Taasisi zinazotoa msaada wa kisheria ili Mkata rufaa aweze kutetewa wakati wa kesi yake.

Hoja nyingine iliyowasilishwa ni kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa je zile zilikuwa ni vipande vya nyama ya swala au laah na Wakili Moses amesema vipo vigezo vinavyoweza kutumiwa na Wataalamu wa kutofautisha nyama ambavyo katika kesi hiyo havikutimika.

Jaji Mgetta aliahirisha shauri hilo hadi February 02,2024 asubuhi ambapo Mawakili upande wa Serikali watawasilisha hoja zao, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi amesema wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwa Watoto wa Maria na ni maombi yao waachiwe huru .

Ikubukwe Mjane Maria Ngoda alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Iringa kifungo cha miaka 22 Jela mnamo November 23 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala.

Leave a Reply