• Sat. Feb 24th, 2024

Nijuzetz

Waambie Wanijue Wanitumie

Serikali yaanza kulifanyia kazi swala la mlima Kitonga, Upanuzi wa barabara waanza kupunguza ajali.

Bynijuzetz

Feb 2, 2024

Hatimaye kilio cha muda mrefu cha Watumiaji wa barabara kuu ya TANZAM kutokea Ruaha Mbuyuni hususani eneo la mlima Kitonga kimeanza kufanyiwa kazi kwa kupanua barabara hiyo kuifanya ya njia nne ili kuepusha foleni za mara mara na kuufanya mlima huo kupitika kiurahisi.

Meneja wa TANROADS Iringa Mhandisi Yudas Msangi amesema ujenzi wa mradi huu utagharimu shilingi bilioni 6.4 hadi kukamilika na itajengwa barabara ya kiwango ya njia nne ambayo itakuwa na mifereji mikubwa ya kuongoza maji na kufungwa vioo vikubwa kwenye kila kona ili kusaidia upishano mzuri wa magari nyakati zote.

Leave a Reply