ARUSHA: KUTOKA IDADI YA 270, WATUMISHI HEWA WENGINE 30 WABAINIKA

ARUSHA: KUTOKA IDADI YA 270, WATUMISHI HEWA WENGINE 30 WABAINIKA

19
0
SHARE

watumishi hewaNa Zuhura Simba

Kutokana na sakata la watumishi hewa katika ofisi za Serikali , kushika hatamu, kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa kubaini idadi ya watumishi hewa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amesema idadi ya watumishi hewa mkoani humo imeongezeka haswa kwenye wilaya mbili za Karatu na Arumeru   kutokana na uchunguzi wa awali na kubaini upotevu wa sh bilioni 1.8.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini  Arusha, Ntibenda alisema wanafuatilia akaunti za watumishi hao hewa na akatoa wito kwa baadhi ya watumishi waliokuwa wakifuja fedha za serikali kwa njia ya udanganyifu,wameombwa wazirejeshe.

Alisema awali wakati timu ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza watumishi hewa ilibaini mkoa huo kuwa na watumishi hewa 270, lakini hadi jana idadi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi ya 300.

“Bado tunaendelea na uchunguzi na naamini wataongezeka lakini hivi sasa hao watumishi hewa wanahaha kurudisha fedha za serikali lakini hata kama wakirudisha watapelekwa mahakamani,” alisema Ntibenda.

Alisema hata kama fedha hizo watazirudisha, lakini watawafikisha mahakamani na pia wanafuatilia kujua ni kwa nini wakuu wa idara zao walifahamu udhaifu huo, lakini walikaa kimya na kuwalipa mishahara huku wakijua kuwa wanaihujumu serikali.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY